TIA NDO MANGOMZIMA. Powered by Blogger.

Sunday, May 26, 2013

BARUA HII KWA WANA TIA






        Hellow tia,
Hope mko poa na mnaendelea na mitihani kama ilivyo ratiba ya chuo, nadhani kila mtu na mwanachuo anaelewa kuwa tarehe 10 mwezi wa tano ni nini ambacho kilitokea pale maisha club ambapo ndipo ilipokuwa fainali ya mr and miss TIA, na washindi kuahidiwa na rais bwana GIFT JENGERA  kuwa zawaadi zao watapewa siku ya ijumaa tatu ambayo ilikuwa tarehe 13 hivyo basi tarifa ni kwamba washindi na washiriki wote hawajapewa zawadi zao kilichoingia hapo ni siasa tu na kupigwa tarehe kama watoto wadogo, kiukweli much respect to Mr prime minister, waziri wa michezo na naibu waziri wa elimu for what you did kwani ulikuwa a washiriki hadi mwisho na ninadhani unaumia sana ila siasa zimeingia, eti mh. hao wandish wa habari bado hawajapatikana ili muwakabidhi zawadi zao kwa mbwembwe nyingi kama mlivyotangaza pale maisha? je mtaingiaje mkataba na kampuni ambayo haina kichwa wala miguu? Je hivi mkataba ulisemaje? na nini  sababu ya kuwa ahidi watoto pesa mtawapa hata za tiaso mdhamini akishindwa kuwapa alafu hamjawapa? hivi makamu wa rais ni nini sababu ya kukisaliti chuo kwa sababu ya kaajira kadogo ulikopewa na kushindwa kutetea haki za wanafunzi ambao walikuweka madarakani na nakumbuka kwenye kampeni zako ulisema we ni mwanamke shupavu na hauteteleki mbona kikazi kidogo hicho kimekutoa kwenye ramani kabisa? Mr Rais unaheshimika sana ila ulitereza kidogo kwa kuweka siasa kwenye suala la utendaji maana shughuli ingebidi imalizike siku ile  hamna zawadi hamna kupanda ni nini hiyo????????????
  Najua jinsi gani jamaa wanavyoumia na wanawaheshimu sasa mnaenda mahakamani kufanya nini wakati maamuzi madogo ya kufata mkataba yaliwashinda na kubakia propaganda tarehe 25 mlioahidi si jana zikuwapi zawadi au kuna kitu kinaendelea nyuma ya pazia nini watu hatujui  maana mmekaa kimya sana hata mkiulizwa mnatoa majibu mepesi sana, tunaelewa haki ya mtu ailiwi  hivyo jitahidini  watu wapewe chao acheni siasa za kitoto, Kinachotakiwa ni zawadi na sio waandishi wa habari maana kila siku tunawaangalia kwenye TV na tunawasikiliza eti wana TIA kuna mtu amfahamu jerry muro hapa?
  Wana tia wanapenda haki sana ila wanaumia kutokana na uzembe ulioonyeshwa na serikali yao ya wanafunzi kutofanya maamuzi magumu kwenye vitu vya msingi kueni makini next time maana kwenye ticket hadi chooni kulikua na matangazo ila zawadi system is loading.... kimyaa kama maji ya mtungi hadi wengine kuwa wasaliti hahaha kweli ushamba ni mzigooooooo, nimeamini kuzaliwa Dar chuo kikuu maana hata kutumia mkataba mnashindwa wakati mmesoma business law.
 Kama kuna mtu anabisha aje aambiwe ukweli na kama kuna ajatendewa haki aende mahakamani kwa kile kichoandikwa hapa.
       Ni mimi mpenda haki mchukia siasa uchwara
 tia@gmail.com