WANAFUNZI wawili wa chuo cha biashara wamepoteza CBE wamekufa
papo hapo kwenye ajali baada ya kugonga tela la mizigo lililokwama
barabarani baada ya kuhalibika.
Ajali hiyo ilitokea jana majira ya saa 1.00 usiku baada ya kugonga
tela la lori la mizigo kwa nyuma wakati wanafunzi hao walipokuwa
wakitokea kwenye mwaliko wa sherehe ya rafiki zao iliyofanyika katika
kijiji cha ihumwa manispaa ya Dodoma.
Gazeti hili lilishuhudia msongamano mkubwa wa magari katika
barabara hiyo iliyopo pembezoni mwa kambi ya jeshi ya Ihumwa kwa
takribani saa zaidi ya tatu kabla ya polisi wa usalama barabarani kufika
na kuongoza utaratibu wa kuondoka.
Kaimu kamanda wa polisi mkoa wa Dodoma Suzan Kaganda alisema chanzo
cha ajali hiyo ni mwendo kasi wa wanafunzi hao wakati wakiendesha
pikipiki hiyo yenye namba za usajili T 420 CCN waliokuwa wakukitokea
barabara ya morogoro kuingia mjini.
Suzan aliwataja kuwa ni Ramadhan Lesso na Gerger Lwandala wanafunzi
wa CBE na kwamba uzembe wa Dereva wa lori hilo lenye namba za usajili T
477 ABM na huku Tela lake ni T 838 AAZ aliyeliacha barabrani zaidi ya
wiki bala kuweka alama yoyote huku matengenezo ya barabara hiyo
yakiendelea katik eneo hilo.
Aliongeza kuwa miili ya marehemu hao iliyokuwa imehalibika vibaya
kutokana na kufumuka fuvu la kichwa cha aliyekua dereva wa pikipiki hiyo
na ubongo kusambaa katika eneo hilo imehifadhiwa katika hospital ya
mkoa.
Kwa picha za ajali hiyo bofya soma zaidi lakini tunaomba radhi kwa picha hizo zinaleta usumbufu ukiziangalia
Miili ya Marehemu Ramadhan Lesso na Gerge Lwandala inaonakana
kabla ya kuondolewa katika kijiji cha Ihumwa barabara ya Morogoro Dodoma
kabala ya kuondolewa na kuhifadhiwa katika chumba cha maiti hospital ya
mkoa.

Baadhi ya watu wakiisogeza miili ya Wanafunzi wa CBE Dodoma
walikufa kutokana na kuligonga tela la lori kwa nyuma kutokana na
mwendo kasi huku lori hilo likiwa limetelekezwa zaidi ya wiki bila alama
yoyote barabarani hapo.

Baadhi ya asikari wa Jeshi la wananchi walionekana kujaribu kutoa
msaada katika ajali hiyo iliyosababisha vifo vya wanafunzi wa chuo cha
biashara CBE Dodoma.

Asikari wa wasalama barabarani akisaidiana kupima upana wa
barabara sehemu ilipotokea ajali hiyo ilihusisha pikipiki na lori la
mizigo. Habari Vyuoni inatoa salamu za rambirambi kwa wanafunzi wote wa
CBE na Mungu awape nguvu katika kipindi hiki kigumu!