Hapa chini kuna muongozo wa kumfanya kijana afanikiwe kimaisha
UNACHOAMINI
Njia
ya kwanza ya kijana kujikomboa inaanzia kwenye kile anachoamini katika
maisha yake. Katika hali ya kawaida mwanzo wa imani ya mwanadamu
hutoka kwa wazazi wake na wakati mwingine mazingira atakayokulia.
Kwa
mfano, wengi tumekuwa na dini kwa sababu tulizaliwa na wenye dini, kwa
maana hiyo hata tunachokiamini hatukuchagua kwa akili zetu wenyewe.
Kwa msingi huo, kama kuna walio na dini mbaya (nataja tu), wengi wao
wameponzwa na kile walichorithishwa na wazazi wao.
Hali iko
hivyo kwenye njia hii ya kwanza ya kijana kuelekea kwenye mafanikio.
Wengi tumezaliwa na kurithishwa imani ya kutofanikiwa. Wazazi wetu
walitulea kwa kutuambia maisha ni magumu, hatuwezi kufanikiwa, sisi ni
masikini, duni na maneno kama hayo ya kukatisha tamaa.
Hata
hivyo, walifika mbali zaidi ya hapo kwa kutuita majina “mbwa, nyani,
wajinga, wapumbavu, vichaa na waliolaaniwa. Ushahidi wa hili upo mpaka
leo, kuna wazazi wanawaita watoto wao majina ya aina hiyo.
Kwa
hiyo, tukakua tukiamini kuwa sisi ni watu duni ambao hatuwezi
kufanikiwa na kama tukiona mafanikio sehemu yoyote tunakuwa na mawazo
kuwa, hiyo ni zawadi ya akina fulani wa ukoo mwingine, lakini siyo
sisi.
Mawazo ya vijana wengi leo yanaamini kuwa, umasikini ni
mzigo mkubwa usiokuwa na ufumbuzi. Kitaalamu mtu anapokuwa na mawazo ya
kutokufanikiwa hawezi kufanikiwa kwa sababu mafanikio huhitaji nguvu
na nguvu za mwili haziwezi kujitokeza kama hazikuvutwa kufanya kazi.
Kwa
msingi huo, ili mtu aweze kufanikiwa lazima mawazo yake yakubali kuwa
mafanikio ni sehemu ya lazima katika maisha. Jambo hili haliwezi
kutokea mpaka kijana mwenyewe aliyelelewa kwenye mawazo ya kushindwa
apigane vita na mawazo ya kutofanikiwa na kuyashinda.
Njia pekee
ya kujikomboa na mawazo mgando ni kufuta na kupuuza kauli zote
alizoambiwa na wazazi wake kuhusu maisha magumu na kuanza kuamini kuwa,
maendeleo ni yake na kwamba muda unahitajika kuyafikia.
Nakushauri
kijana mwenzangu kuanzia leo uyakatae mawazo ya kushindwa na kukubali
udhaifu wako kwamba huwezi kufanikiwa kwa sababu yoyote ile, sema
LAZIMA UFANIKIWE KWA KUWA UWEZO HUO UNAO.
UNACHOTENDA
Ukiangalia
tabia ya maisha ya mwanadamu utagundua kuwa anafahamu mambo mengi
sana, lakini hatendi sawa na ufahamu wake. Naamini hata vijana wanajua
njia za kufanikiwa, lakini hawazifuati.